GET /api/v0.1/hansard/entries/667393/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 667393,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/667393/?format=api",
"text_counter": 93,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Wabunge watakuwa ili nao wapate nafasi ya kutoa mchango wao. Ninatumai ndugu yangu, Mheshimwa Duale, ambaye anaondoka atafahamu kuwa sikuwa ninasubiri Wabunge wawe hapa tu ila hali ilivyokuwa kwa wakati huo ilibidi Wabunge nao wajitolee na kutoa mchango wao. Mhe. Spika, nchi hii haiwezi kuendelea kama barabara hazijafadhiliwa na kufunguliwa. Pia, nchi hii haiwezi kuendelea kama barabara zitakuwa upande mmoja. Nchi hii haiwezi kuendelea iwapo sehemu tofauti tofauti zitakuwa na barabara zisizofanana. Eneo Bunge la Wundanyi lina nusu kilomita ya barabara ya lami tangu tupate Uhuru. Ukienda kwingine, lami imetamba kila mahali. Mhe. Spika, ni ombi na maoni yangu kuwa kitengo hiki kifadhiliwe na kushikiliwa vizuri. Serikali ikiweka pesa za kutosha na waliochaguliwa kukiongoza wawe imara, kitengo kitatoa mchango wa kutosha katika nchi hii. Hali ilivyo, tunaona barabara zetu zimekumbwa na matatizo. La kwanza ni utekelezaji wa ujenzi wa barabara. Utakuta kuwa wanaopewa nafasi za kujenga hizo barabara wana kasoro nyingi. Ni kwa sababu hatuangalii iwapo hizo barabara zinajengwa sawa. Barabara hizo zinabomoka muda mfupi baada ya kujengwa. Utajiuliza waliokuwa na kazi ya kufanya na waliopewa majukumu ya kusimamia barabara hizo ni nani. Pili, kampuni zinazoshughulikia barabara zetu ni za Uchina. Swali ninalotaka tujiulize ni iwapo kampuni hizi za Uchina zimebainika wazi kuwa na uwezo na uzoefu wa kututengenezea barabara tukilinganisha na kampuni zilizokuwa hapo awali za Uingereza, Ujeremani au Waafrika wenzetu, shida iko wapi? Tatu, ni matumizi ya barabara. Kuna barabara zilizojengwa zitumiwe na magari ya uzani fulani. Mara nyingi, utakuta magari yanayotumia barabara hizo yameachiliwa kuziharibu. Unakuta barabara kama hiyo inadumu kwa miaka mitano, kumi au sita ilhali iliundwa idumu kwa miaka 30. Walio na majukumu kuhakikisha barabara zinatumiwa na magari ya uzani uliokubalika hawafuati sheria hizo. Tutaendelea kutumia pesa za umma kwa muda gani ndipo Wakenya wajue kuna upotevu fulani? Katika Bajeti tunayoitumia wakati huu na makadirio ya fedha tutakazoziweka kwenye barabara, Wizara ya Uchukuzi na Miundo Msingi imepewa kiwango kikubwa sana cha pesa. Barabara ziko wapi? Wakati umefika tuambiane wazi wazi kuwa hii nchi inahitaji barabara kwa usawa. Isiwe barabara zinazotakiwa kutengenezwa kwa muda uliopeanwa hazitengenezwi. Tumeisubiri barabara ya Taveta hadi Voi kwa miaka mingi. Ninashukuru inakaribia kumalizika. Hata hivyo, watakikanao kufadhiliwa kwa kutoa mashamba yao kwa mradi huo kutoka Bura hadi Mwatate hawajalipwa hadi sasa. Tunaomba wanaohusika kuhakikisha wenyewe wamelipwa ili barabara ipewe nafasi kupita kwa muda uliotegwa. Tunasema heko kwa Serikali kwa sababu hatukuwa na hiyo barabara kwa muda huo wote. Tunasisitiza kuwa barabara ya kutoka Mwatate hadi Wundanyi na Wundanyi hadi Bura kupitia Werugha na Mghange iwekwe maanani itekelezwe na ijengwe kama nyingine. Barabara ya kutoka Voi hadi Mombasa ina pahali parefu sana pa mchanga. Imebainika wazi ajali nyingi zinatokea hapo. Tunaomba wanaohusika kuhakikisha kuwa barabara hiyo inamalizika. Nikisoma Mswada huu, ninaona kuna watu wameombwa kuhusika kwa uendeshaji wa Bodi. Wahasibu wanahitajika. Nimeona kipengele kinachotaka mhasibu awepo kwenye Bodi. Nilisikia mmoja wetu akisema haoini faida ya mhasibu ndani ya Bodi. Makadirio ya barabara na utekelezaji wa shughuli zote unahitaji hesabu sahihi. Atakayetupa hesabu sahihi ni nani kama si mhasibu? Ijapokuwa taaluma zingine pia zinahitajika, hatuwezi kuiwacha ya uhasibu nje. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}