GET /api/v0.1/hansard/entries/667436/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 667436,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/667436/?format=api",
"text_counter": 136,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Kama Wabunge, Mswada huu utatupa mwangaza kutekeleza majukumu yetu ya kuangalia jinsi hela inatumika pande zote mbili - Serikali kuu na serikali za kaunti - kinyume na vile magavana wanavyofikiria kwamba sisi hatupaswi kuchunguza matumizi ya pesa katika kaunti. Mhe. Spika, ni jambo la kusikitisha. Ilifikia kiwango kwamba barabara zetu zilizorota kwa sababu ya mvutano. Tumekuwa tukitetea barabara nyingi zisimamiwe na Wabunge. Kuna mfano mzuri wa matumizi mabaya ya pesa pale ambapo magavana waliamua kuchukua hospitali zote na hivi leo, hospitali hazina madawa. Kunguni tele na watu wanalala watano na wengine wanalala chini. Hivi sasa, wamepewa nafasi ya kusimamia barabara na sisi pia tuna hofu iwapo wataweza kusimamia vizuri kwa sababu lengo lao sio kumuhudumia mwananchi, bali ni kuweka pesa mifukoni. Mhe. Spika, kuna tatizo kuu katika Kaunti yetu ya Kwale. Tumekuwa tukiambiwa kuwa Dongo Kundu itajengwa barabara. Ingekuwa imejengwa. Lile tatizo la watu na magari kutumbukia baharini lingekuwa limeepukika. Ule msongamano ambao uko katika feri ni kwa sababu Dongo Kundu imekuwa ni nyimbo au hadithi ambayo mpaka leo haijawahi kutekelezwa. Tuna imani kwamba kupitia Mswada huu, barabara nyingine kama hiyo ya Dongo Kundu, ile iliyoko eneo Bunge la Matuga, na ile iliyoko Marere kuzunguka kupitia Shimba Hills hadi Mabungo, imewekwa lami kwa wakati unaofaa. Barabara hiyo katika Eneo Bunge la Matuga imesaidia usafiri na ingeweza kusaidia kusafirisha mazao na hata wagonjwa. Hufikia kiwango ikawa barabara hiyo haipitiki. Barabara nyingine ni ile ya Samburu-Kinango-Kwale-Lungalunga The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}