GET /api/v0.1/hansard/entries/667437/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 667437,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/667437/?format=api",
    "text_counter": 137,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "kupitia Ndavaya. Hivi sasa, magari yote kutoka Tanzania yanatumia barabara hiyo kwa sababu yanapopitia feri, inachukua siku tatu au nne ndio gari liweze kuvukishwa. Barabara ya Samburu- Kinango-Lungalunga imerahisisha usafiri. Kwa upande wa utalii, barabara hiyo ya Samburu- Kinango-Lungalunga-Kwale inafaa kuwekwa lami wakati huu. Hii ni kwa sababu imekuwa nyimbo tangu enzi ya Rais Mstaafu Daniel Arap Moi. Kila wakati tunaambiwa kwamba lami itawekwa, lakini hatujawahi kuiona. Sasa hivi, tunategemea barabara hiyo kwa utalii. Ikiwekwa lami, itatufungulia utalii ambao umezoroteka katika Kaunti yetu ya Kwale."
}