GET /api/v0.1/hansard/entries/667438/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 667438,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/667438/?format=api",
"text_counter": 138,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Barabara iliyo katika eneo la Lungalunga inayoenda Shimoni ni barabara nyingine muhimu. Hivi leo, tunataka bandari ijengwe haraka lakini ikiwa barabara kutoka Kanana hadi Shimoni haitawekwa lami, basi hakutakuwa na maana. Mvua inaponyesha, barabara hiyo haipitiki. Barabara ya kwenda Vanga pia haipitiki mvua inaponyesha. Sehemu hizi ni nzuri sana katika kukuza utalii katika eneo letu la Kwale. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu utatuonyesha mwelekeo ambao utatekeleza mahitaji muhimu ya mwananchi."
}