GET /api/v0.1/hansard/entries/667990/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 667990,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/667990/?format=api",
"text_counter": 201,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili nami nichangie Hoja iliyo mbele yetu. Kwanza, ningependa kutoa kongole kwa ndugu yangu Yusuf kwa kuweza kutupa kofi ya fahamu. Mheshimiwa Yusuf ametupiga kofi ya fahamu na ametuzindua tuweze kuishukuru historia ya taifa la Kenya. Utakapoangalia kwa uchache wa fikra, Hoja iliyo mbele yetu haina maana. Lakini utakapokwenda kwa bahari na upana, utakapofurahia historia ya taifa lako na kumbukumbu ya kule tulikotoka, Hoja iliyo mbele yetu ni muhimu na inastahili kuungwa mkono na kupitishwa ili sehemu hiyo iweze kuhifadhiwa iwe katika kumbukumbu ya taifa ama katika makavazi ya taifa. Ninasema hivyo kwa sababu mapambano ya vita vya Uhuru ni kama tumevuka hatua ya kwanza lakini mapambano ya haki ya Wakenya bado iko. Leo sisi tunasherehekea kuwa na Rais kama Uhuru Kenyatta, ambaye anatambua haki na anawatambua Wakenya kwa upana. Lakini kesho atakapokuja dhalimu, dawa ya dhuluma ni Kamukunji. Tutakutana na wao vile tulivyokutana na Rais mstaafu Moi na tukabadilisha Kipengele cha 2(a). Kiwanja cha Kamukunji kitatumika kupambana na yeyote atakayejaribu kuwapeleka Wakenya vibaya na tutakwenda kumutuliza katika kiwanja cha Kamukunji. Mimi saa zingine ninavunjwa moyo na tabia ya Wakenya. Wakenya hawatambui wala kuheshimu mashujaa waliotoa mhanga nafsi zao na waliomwaga damu ili taifa la Kenya lipate Uhuru. Angalia raslimali ambayo nchi hii iko nayo leo, hata kalkuleta zilizotengenezwa na wanasayansi leo hazitumiki tena mpaka kalkuleta mpya itafutwe kwa sababu uchumi umeenda The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}