GET /api/v0.1/hansard/entries/667991/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 667991,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/667991/?format=api",
"text_counter": 202,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "kiasi ya kufika trilioni. Katika hii trilioni, raslimali ngapi tumetenga kando kwa minajili ya wale waliopigania Uhuru wa taifa hili? Hawa mashujaa wamekuwa masikini kuliko masikini wengine wote. Watoto wao na wajukuu wao wako katika hali mbaya. Tumetenga pesa gani kulinda haki ya wale mashujaa wachache waliopigania Uhuru wa Kenya? Badala yake, tunaraukia kitendawili kila asubuhi ambacho hakiweki ugali mezani. Kwa aibu kubwa, Wakenya wameenda Ethiopia kuleta mtu anayeitwa Elema Ayanu, ambaye ni “ndugu” yangu. Yeye ni Oromo. Mimi naye tunaongea lugha moja. Kama atakuwa shujaa, atakuwa shujaa Ethiopia sio Kenya. Angalia wale mashujaa ambao tuko nao humu nchini, wako hali gani? Tunawakandamiza, tunawadhalalisha na kuwaacha vile walivyo. Badala yake, tunakwenda kumleta mwananchi wa Ethiopia na kupiga mlolongo kutoka uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, barabara zinafungwa mpaka mjini kwa sababu Elema Ayanu amebebwa. Kabla hujamleta Elema Ayanu kutoka Ethiopia, wale walioko nasi Nairobi umewafanyia nini? Kwa hivyo, inanisikitisha sana. Hatutambui historia yetu na mashujaa wetu. Hatuna mikakati ya kuhifadhi mashujaa na taasisi ya historia ya Kenya."
}