GET /api/v0.1/hansard/entries/668006/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 668006,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/668006/?format=api",
"text_counter": 217,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza, ninataka kumpongeza Mhe.Yusuf kwa kutuletea Hoja hii ambayo inatupatia historia yetu kama Wakenya. Tunatakikana kuzingatia Hoja hii. Pengine wengine wanaona ni Hoja isiyokuwa na uzito lakini ina uzito sana haswa tukiangalia kuwa lazima tuwe tunajiashiria na kuambia vizazi vyetu pale tulipotoka. Tunaona viongozi wengi wetu ambao sasa wako mbele katika utetezi wa haki, walitetea nchi yetu kwa kupambana na wale wabeberu mpaka sisi tukapata Uhuru. Kiwanja hiki kilikuwa mojawapo ya viwanja ambavyo watu walikuwa wakikutana wakitathmini na wakizungumzia njia mwafaka ya kutupa ukombozi. Kiwanja hiki lazima kiangaliwe na kuwekewa hadhi, kuhifadhiwa na kuwekwa mapambo ambayo yataashiria historia. Tunataka tukiangalie kama vile ambavyo tumeangalia taasisi za kihistoria. Kule Pwani, tuna taaasisi ya Fort Jesus ambayo imehifadhiwa na kulindwa kwa sababu inatuonyesha historia za Mreno na Mwingereza walipokuja pale Mombasa. Hivyo basi, vizazi na nchi nyingi sana hutembea pale na kulipa ada za fedha ili kusoma historia hiyo. Kiwanja hiki ikiwa kitaangaliwa katika hali ya kuhifadhi historia yetu na pia kuweza kukilinda, wale ambao wanapenda kunyakua ama kuweka mijengo karibu na viwanja kama vivyo, hawatafaulu. Pia kinaweza kutengeneza ajira ndogo kwa vijana ama Wakenya wengine kwa sababu kitatengenezwa na kuweka wasimamizi ili sura yake halisi iweze kuhifadhika The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}