GET /api/v0.1/hansard/entries/668007/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 668007,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/668007/?format=api",
"text_counter": 218,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "ndiposa unaposema ni kiwanja cha historia, kila mmoja ataweza kukijua. Tuweze kupata zile pambo mwafaka za kuwekwa pale na majina ya wale mashujaa wetu ambao wamepigania Uhuru wetu. Kama vile mwenzangu, Mhe. Ali, amesema, sisi tumewasahau mashujaa wetu. Juzi nilikuwa America na tukatembea sehemu ya Rhode Island mahali ambapo kunajengwa nyumba nyingi, takriban nyumba 200 za wale waliopigania uhuru. Kumejengwa nyumba za kisasa ambapo wamewekewa makanisa, benki na hao mashujaa wamewekewa mnara wa historia yao. Hapa kwetu tunawakumbuka tu wakati tuna siku zetu mwafaka za kihistoria kama Madaraka Day na tunasema tunawakumbuka wale waliopigania Uhuru. Tunapokumbuka siku hizi za kihistoria, inafaa tuwapatie mashujaa wetu heshima na kuwaweka katika njia itakayowapatia hadhi kwa kazi waliofanya. Ninaunga mkono swala hili kwa sababu vizazi vyetu vichanga ambavyo viko sasa, ikiwa vitaweza kutembelea sehemu kama hizi na kuelezewa historia ya viwanja kama hivi, vitaweza kujenga uzalendo. Uzalendo ni jambo ambalo linaingia katika nafsi ya mtu na kumpatia ari na Uhuru katika nafsi yake kujua kwamba yeye ni mzalendo. Uzalendo unaletwa na historia zetu. Tujue pahali tunapotoka na baada ya kupata Uhuru, watu wamepigania haki za kibinadamu. Kiwanja hiki kimetumika sana. Mpaka sasa, watu wanaopigania haki za uhuru kama Maina Kiai, Khalif kutoka Pwani na wengine wamekuwa wakitumia viwanja hivi. Hivyo basi, inafaa tukae katika viwanja kama tunapofanya maombi ya kitaifa haswa kwa wakati huu ambapo tunaelekea wakati wa uchaguzi. Lazima tuonyeshe uzalendo kama Wakenya na tujenge nchi yetu. Njia moja ya kutuweka pamoja ni kutumia viwanja vya kihistoria kama hivi ambavyo wakati ukiwa pale, unajikumbusha, unapata kumbukumbu na unajua tumetoka wapi. Baada ya kutembea pale, tutapiga hatua ya kutorejea kule nyuma kwenye giza"
}