GET /api/v0.1/hansard/entries/668009/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 668009,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/668009/?format=api",
    "text_counter": 220,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Hivi sasa, kule Pwani tuko na Uhuru Gardens. Uhuru Gardens itabaki Uhuru Gardens na tutaihifadhi, tutaingalia na tutailinda. Kule magharibi, kuna Masinde Muliro Gardens ambayo itabaki kama Masinde Muliro Gardens kwa sababu hiyo ni historia. Ni lazima tuhifadhi kiwanja cha Kamukunji, tukilinde and kukipatia hadhi inayohitajika ili vizazi vyetu vichanga na wageni wanaokuja wajue pahali Wakenya walitoka, wanakoelekea na jinsi watakavyoendelea kujenga Kenya. Kwa hayo mengi ama machache, ninaunga mkono Hoja hii. Pia, ni lazima tuangalie vile viwanja vingine katika Jamhuri yetu ya Kenya ambavyo vinatakikana kuwekwa katika hali ya kitaifa na hali ya kihistoria ili historia yetu ihifadhiwe na tuzidishe uzalendo wetu kama Wakenya."
}