GET /api/v0.1/hansard/entries/668048/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 668048,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/668048/?format=api",
"text_counter": 259,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wekesa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2742,
"legal_name": "David Wafula Wekesa",
"slug": "david-wafula-wekesa"
},
"content": "Asante sana Mhe. Yusuf. Hongera kwa kuileta Hoja hii. Mhe. Aliileta Hoja hii kwa kuzingatia kwamba eneo lake la Bunge linatokana na jina “Kamukunji”. Sehemu nyingi hapa nchini hasa sehemu za mijini zinajulikana kwa jina “Kamukunji”. Ajabu ni kwamba watu wengi hawajui umuhimu ama maana ya jina “Kamukunji.” Nilipokuwa naongea na Mhe. Hassan, aliniambia kwamba Kamukunji isionekane kuwa ndogo. Ni sehemu kubwa ambayo imenyakuliwa. Ni ajabu kuwa sisi kama viongozi tunakaa hapa, sehemu muhimu zinanyakuliwa na tumenyamaza. Sio tu Kamukunji, ni sehemu nyingi za aina hii ambazo zimenyakuliwa. Wengi wetu ambao tumepata nafasi ya kupitia sehemu ya Kamukunji hupigwa na butwaa tukiona hali ya mazingira yake ikilinganishwa na vile ambavyo “Kamukunji” inavuma. Ingekuwa vizuri kama Serikali ingefanya sehemu hiyo iwe mojawapo ya sehemu za ukumbusho wa kitaifa. Naunga mkono Hoja hii."
}