GET /api/v0.1/hansard/entries/668911/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 668911,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/668911/?format=api",
"text_counter": 153,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 128,
"legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
"slug": "richard-onyonka"
},
"content": "Asante, Mheshimiwa Spika kwa kunipa fursa ya kuchangia Hoja hii. Nimeangalia orodha ambayo Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Mipango na Biashara ameleta na sijaridhika sana. Sababu ni kuwa ukiangalia orodha yenyewe, idadi ya akina mama ambao wako hapo ingekuwa juu kidogo kulingana na vile ambavyo Katiba inasema. Jambo la pili ni kuwa Katiba yetu inasema kuwa kama kuna Wakenya lazima wapewe kazi, kabla Bunge lipitishe majina hayo, lazima tuzingatie kama Wakenya hao wametoka katika maeneo yote ya Kenya. Ukizingatia masuala yaliyo nchini wakati huu, utapata kuwa ingekuwa vizuri tuwe na uwiano, upendano na uelewano ambapo kila Mkenya anahisi kuwa yeye ni Mkenya. Majina yaliyo hapa hayaonyeshi kuwa hawa jamaa waliopewa kazi hii wametoka kutoka pande zote za Kenya. Sisemi kuwa lazima watoke katika kila kabila la Kenya lakini hata afueni ingewezekana ndugu yangu, Mwenyekiti, ajaribu kidogo amtoe mtu mmoja Pwani, mwingine kutoka Nyanza, mwingine kutoka Kaskazini mwa Kenya, mwingine kutoka Mkoa wa Kati na mwingine kutoka Kaskazini Mashariki. Angefanya hivyo, ingeonyesha uso wa Kenya. Mimi sitakubali majina haya yapitishwe. Ingekuwa vizuri kama Kamati za Bunge zingetilia maanani Katiba yetu ya Kenya ambayo inasema ni vizuri tuifuatilie ili Kenya iwe nchi ambayo tunapendana."
}