GET /api/v0.1/hansard/entries/669340/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 669340,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/669340/?format=api",
    "text_counter": 99,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwakulegwa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 101,
        "legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
        "slug": "danson-mwazo"
    },
    "content": "Bw. Spika, ninaunga mkono Hoja hii. Heko kwa akina mama kwa sababu Katiba yetu imewapa nafasi katika shughuli zetu za ujenzi wa taifa. Kwa mfano, Seneti hii ina Maseneta 18 wa kike walioteuliwa kwa sababu ya Katiba yetu. . Tunajua ya kwamba kuna akina mama waliogombea kiti cha urais katika nchini. Hawa ni Mhe Ngilu, Mhe. Karua na Mhe. Nazlin. Hii ni kwa sababu hakuna unyanyasaji wa kisiasa na Katiba yetu inampa kila mtu haki ya kugombea kiti chochote nchini. Ninawasihi akina mama kujitoa mhanga na kugombea viti vyote vya kisiasa bila kungojea kutengewa viti fulani. Tuna mifano mingi ambako akina mama baada ya kuteuliwa kwa muda wa miaka mitano, wao hujipigia debe hadi kuchaguliwa. Ni lazima akina mama viongozi hapa nchini wapange kongamano na akina mama wa mashambani ili wawaeleze umuhimu wa kungombea viti vyote vya kisiasa. Viwanda vingi ambavyo vinasimamiwa na akina mama vimeimarika sana. Mama Tabitha Karanja wa Keroche Breweries ni mfano mzuri wa akina mama waofanya vizuri. Amekiongoza kiwanda hicho hadi kufikia ngazi za kimataifa. Ni lazima akina mama wa mashinani waelemishwa kuhusu nafasi ambazo Katiba yetu imewatengea ili wawe na ukakamavu wa kugombea viti vyote vya kisiasa. Hapa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}