GET /api/v0.1/hansard/entries/669342/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 669342,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/669342/?format=api",
    "text_counter": 101,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kwetu inawezekana mwanamke kugombea kiti cha urais kama kule Marekani. Akina mama wajitokeze kwa wingi na kuunga mkono mmoja wao. Wakati wa harakati za kupigania Uhuru wa nchi yetu kulikuwa na mama mashuhughuli kutoka Pwani kwa jina la Mekatilili wa Menza. Aliwaongoza watu wa Pwani kupigana na Waingereza waliotaka kunyakua mashamba yao kwa nguvu. Alikuwa na kipawa cha kuwaleta watu pamoja ili wapiganie haki zao. Kwa hivyo, naomba akina mama wajitolee mhanga waweze kupigania haki yao katika taifa hili. Wasingojee kupewa viti bure kwani hatuna viti vingi. Ni lazima wagombee viti vya ubunge, useneta na vingine vyote. Ninaomba akina mama kujitolewa kwa wingi katika uchaguzi ujao ili wawezekupigania viti vingi. Inafaa viti vyote viwe wazi, na akina mama wajisatiti ili wakienda katika kura wawe na mikakati mizuri. Bw. Spika, ninaunga Hoja hii mkono."
}