GET /api/v0.1/hansard/entries/670128/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 670128,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/670128/?format=api",
"text_counter": 25,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Nasahihishwa kuwa ni Mhe. wa Igembe ya Kati, samahani. Kitengo cha ndugu zetu ambao wanashughulika na wanyama wa pori kinauzoefu wa kujisongeshea ardhi kiholela. Kwa mfano, kule Taita, kutoka Maungu hadi Voi, upande wa chini wa reli, katika mwaka wa 2009, KWS ilijisongeshea ardhi ambayo ni ya wananchi. Watu wa sehemu hiyo wamepitisha ombi lao na litakuja kwa Spika. Ukienda Tsavo, pale ambapo watu walishambuliwa na Simba wakati wa kujenga reli kuu, KWS imefanya dhuluma hizo. Pia, imefanya dhuluma katika sehemu za Taveta. Tukienda Kishushe, wameweka ua ambalo sila stima lakini wameliingiza ndani ya ardhi ya wananchi. Hawakuweka ua upande wao. Ukiwauliza, wanakwambia wameamua."
}