GET /api/v0.1/hansard/entries/670131/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 670131,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/670131/?format=api",
"text_counter": 28,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadime",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika, kwa hii fursa ambayo umenipatia. Ninasimama kumuunga mkono Mbunge wa Igembe ya Kati kwa haya malalamishi ambayo ameleta kwa niamba ya wananchi wake. Ni kweli Wizara inayohusika na wanyama pori ina tabia ya kuchukua ardhi ya wananchi. Ombi langu pia lipo njiani. Kuna malalamishi kutoka watu wa Taita Taveta. Walikuwa na malumbano kwa sababu Wizara inayohusika imechukua ardhi yao kama vile Mhe. aliyenitangulia wa Wundayi amesema. Kutoka Maungu, Voi, Tsavo, Taveta na sehemu za Mwatate, KWS imechukua ardhi kubwa sana ya wananchi. Tuliuliza Wizara inayohusika itengeneze jopo ambalo linahusisha wananchi wa hapo na maafisa wa Serikali ili wajaribu kutatua mzozo huo. Lakini jambo hili limechukua muda. Ni vyema Kamati ya Bunge inayohusika ijaribu kuyatatua maswala kama haya ambayo yameletwa na Mbunge wa Igembe ya Kati. Pia, inafaa kuangalia maswala katika mbuga za wanyama nchini na kuyatatua kwa haraka iwezekanavyo."
}