GET /api/v0.1/hansard/entries/670303/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 670303,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/670303/?format=api",
    "text_counter": 200,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mtengo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13164,
        "legal_name": "Willy Mtengo",
        "slug": "willy-mtengo"
    },
    "content": "Tumeona Serikali ikijaribu kuweka himizo sana kwa kuboresha sekta hii. Najua kuna chuo cha Serikali ambacho ni cha mafunzo ya uvuvi wa samaki. Lakini, chuo hiki hakitoshi kwa sababu ni kimoja. Na kama vile Mhe. aliyenitangulia alivyozugumza, chuo hiki kinafunza mafunzo ya taaluma ya juu sana. Tunataka chuo ambacho kinafunza wavuvi mambo ya kawaida. Je tutawafanyia nini wale ambao wanaingia ndani ya madau kwenda baharini kuvua samaki? Sisi hatuna rasilimali nyingine maeneo tunayotoka. Tuna uvuvi peke yake. Kwa hivyo, tunaunga mkono Hoja hii ya kuleta vyuo na tutavisaidia. Niko tayari kutoa ardhi sehemu ya Malindi ya kujenga vyuo. Tuko na ardhi ya kutosha. Tuko tayari kupeana ardhi mradi tuone vyuo vimekuja. Wavuvi wetu wamerudishwa kwa hali ya uvuvi wa leo na kesho. Utunzaji na uhifadhi wetu wa samaki ni leo kwa kesho. Hatuna namna ya kuweka samaki wetu kwa muda mrefu kwa sababu hatuna mafunzo yale ama vigezo vya kutusaidia kwa viwango vile. Kwa hivyo sisi tunaunga mkono Hoja hii na kusema kuwa tunatamaushwa na yale wenzangu waliotangulia kusema kwamba tunapata samaki kutoka China."
}