GET /api/v0.1/hansard/entries/670370/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 670370,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/670370/?format=api",
    "text_counter": 267,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2308,
        "legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
        "slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nakubali kwamba mvumilivu hula mbivu. Kuna watu wamebofya saa mbili baada yangu na wamepata nafasi. Kwa hivyo, ni kuvumilia. Nachukua nafasi hii nikupongeze, nimpongeze aliyeleta Hoja hii na yule aliyeuunga mkono kwa mara ya kwanza. Serikali na watu wanalalamika kwa ukosefu wa kazi. Lau Serikali ingalikuwa inatia bidii na kuzingatia masuala ya uvuvi katika nchi hii, upungufu wa kazi ungalipungua kiasi kikubwa mno. Kwa sababu Serikali imeweka mkono nyuma, mambo haya yanaharibika. Watu haswa walio sehemu zilizo na maumbo makubwa ya maji kama Ziwa Victoria, Ziwa Naivasha na Bahari ya Hindi kule Pwani wanapata shida sana. Iko haja kubwa sana kwa Serikali hii kuhakikisha inapeleka watu wake masomoni kupata nafasi na taaluma ya kuwa na uvuvi wa kisasa. Alivyozungumza mmoja wetu, watu wamebaki wanatumia vifaa vya zamani. Kule kwetu Matuga, watu bado wanatumia neti za kulalia vitandani, majarife na matole yatengenezwayo kwa miyaa. Matole haya yakiingizwa kwa bahari huoza baada ya muda mfupi na samaki hupata nafasi wakapenya na kuhepa. Hii yote ni kwa sababu ya kuzorora kwa Serikali isiyotaka kuangalia watu wake vilivyo. Naiuliza Serikali hii ihakikishe inafanya kila iwezavyo ili watu wa zile sehemu zilizoathiriwa na vitu kama hivyo wapate mafunzo ya hali ya juu wafanye kazi hii kwa njia nzuri mno. Ni jambo la kusikitisha ya kwamba tumepata Uhuru kutoka 1963 lakini tunashindwa hata na watu wa Afrika Kusini waliopata uhuru wao juzi. Juzi nimekuwa Afrika Kusini na nikaona uvuvi ni wa hali ya juu. Nilisema nitamuambia Mhe. Spika ahakikishe anapeleka watu kule, Singapore na kadhalika ilil wapate elimu zaidi. Hiyo ni muhimu ili watu wapate nafasi za kazi kwa wingi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}