GET /api/v0.1/hansard/entries/671158/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 671158,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/671158/?format=api",
    "text_counter": 58,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Spika, namshukuru Sen. (Dr.) Khalwale kwa kuwasilisha masaibu ya watu wa Kaunti ya Isiolo katika Bunge la Seneti. Nchi hii inaelekea ukingoni; taifa karibu liporomoke. Leo, ni wazi kwamba magavana wote na watumishi wengine wa serikali wanapora na kuharibu mali ya taifa hili. Imechukua miaka nenda miaka rudi kabla mmoja wao kupelekwa kortini. Polisi wa Kenya wana uwezo mkubwa sana wa kukimbizana na mtu ambaye amesimama mkutanoni na kusema kwamba kuna wezi katika taifa hili. Huyo mtu anakamatwa 6.00 p.m.; 6.00 p.m. yuko kortini na 7.00 p.m. amewekwa ndani bila mashtaka. Lakini wezi na waporaji wanatembea barabarani huru bila kusumbuliwa na mtu yeyote. Wakati umefika tutetee na kusimamia maslahi ya Wakenya."
}