GET /api/v0.1/hansard/entries/671336/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 671336,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/671336/?format=api",
"text_counter": 236,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante Bwana Spika wa Muda. Naunga mkono Maseneta wenzangu, na wakili wote Kenya nzima. Natoa rambirambi zangu kwa familia ya wakili Willie Kimani. Nashtumu vikali sana ya kwamba ilikuwa ni makosa, kinyume cha sheria kuweza kumchukua wakili, mteja wake na dereva wa texi na hatimaye tumeona ya kwamba kitendo kilichotendeka hapo, kilikuwa cha kinyama sana. Bw. Spika wa Muda, hili ni jambo la taharuki sana katika Kenya yetu. Tumeanza kushuhudia uzembe katika idara ya polisi na hii si mara ya kwanza, ya pili wala ya tatu. Ni lazima hatua ichukuliwe ili idara ya polisi irekebike vilivyo kulingana na sheria za Kenya. Tunategemea polisi kulinda maisha ya mwananchi. Kwa hivyo, hatutarajii polisi wauwe mwananchi ambaye wanatakikana kumlinda. Ni nani atakayelinda mwingine ikiwa Utumishi kwa Wote sasa umekuwa utumishi wa kuua wananchi wa Kenya? Ikiwa wakili anafanya kazi ya kutetea mteja wake na kufungwa mikono nyuma na miguu, akapigwa na kuawa kisha akatupwa ndani ya gunia na hatimaye akakatwakatwa na mwishowe mwili wake ukapatikana ndani ---"
}