GET /api/v0.1/hansard/entries/67271/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 67271,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/67271/?format=api",
"text_counter": 230,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ms. Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Nipe nafasi ili nimalize kuuliza swali langu halafu mtauliza yenu! Nasema hivyo kwa sababu tunatoka pahali watu wanaumia; tunatoka pahali watu wanadanganywa kila siku. Mkisema boreholes zitajengwa, magari ya jeshi yanaenda na wananchi wanayaangalia hayo magari na hakuna kitu ambacho kinafanyika. Kwa hivyo, tunaomba kujua kama kuna chakula ama hakuna. Serikali inasaidia watu wachache. Tunataka waache kudanganya hapa kwamba chakula na maji yatapelekwa huko wakati ambapo hakuna kitu kinachotendeka. Watu wanaumia! Wanafunzi hawaendi shule. Wale wanaotarajia kwenda Form I, hawataenda kwa sababu ya taabu. Kwa hivyo, ningependa kuuunga mkono kwamba kutembea kwa Prime Minister sehemu zile ni kutembelea watu wake wa ODM. Hakuenda kuangalia mambo ya njaa!"
}