GET /api/v0.1/hansard/entries/673161/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 673161,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/673161/?format=api",
    "text_counter": 28,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Dr. Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Mheshimiwa Spika, nikizitoa rambirambi zangu kwa maafisa wetu wa askari waliouawa huko Kapenguria, nina maswali kadhaa kichwani. Tunajifunza nini hapa Kenya kila tupatapo mkasa kama huu? Imekuwa desturi kwamba mkasa wa majambazi kama hawa ukitokea, kazi yetu ni kulia na kusaga meno. Tunapotoa rambirambi zetu na kuwazika walioaga, mambo yanaishia hapo. Kwa hivyo, ni wajibu wa Serikali kwamba kila kutokeapo jambo kama hili, kuwe na funzo fulani ambalo litakumbukwa na kutoa tahadhari mkasa kama huo usitokee tena. Kama kituo cha polisi kinaweza kuvamiwa hivyo, mwananchi wa kawaida ana usalama? Hali ya usalama iko vipi? Hili ni jambo la kutia maanani; si jambo ndogo. Serikali iwe macho na ijipige konde kuchunguza panapo udhaifu katika uongozi na minajili ya mipango ya usalama nchini."
}