GET /api/v0.1/hansard/entries/674136/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 674136,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/674136/?format=api",
"text_counter": 380,
"type": "speech",
"speaker_name": "July 19, 2016 SENATE DEBATES 49 Sen. Bule",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, kwanza, nampongeza aliyeleta Mswada huu kwa sababu ni muhimu sana. Haya si mambo ya kufanya kwa haraka. Kwa hivyo, ni vyema tuyaangalie kwa undani. Ninawakilisha watu wa Kaunti ya Tana River ambao wengi wao hawakuwa wanawakilishwa kisawa. Jambo kama hili linafaa kuangaliwa kwa undani. Katiba mpya ililetwa kwa sababu machifu hawakuwa wanawakilisha vyema wananchi. Walifaa kuwawakilisha wananchi, kujua shida zao na kuziwasilisha kwa Serikali lakini hawakuelewa kazi yao ni nini. Ninapinga baadhi ya vipengee katika Mswada huu kwa mfano sehemu inayosema kwamba machifu watafutwa kazi. Ni lazima tuangalie jambo hili kwa undani kwa sababu machifu hawakuajiriwa ili kuwakilisha magavana. Hata hivyo, wamekuwa wakitumika vibaya na magavana ambao wametumia vibaya fedha za kufanyia maendeleo katika kaunti zetu. Kwa hivyo, ni lazima tuangalie mambo hayo kwa sababu machifu waliteuliwa kutoka kwa wananchi na ni wananchi wanaolalamika kwamba machifu hawahitajiki tena. Mtu yeyote anayewakilisha wananchi, awe chifu, mkuu wa taarafa au mkuu wa wilaya, lazima aelezwe kwa uwazi kuwa hakuajiriwa kumwakilisha gavana na kuendeleza unyakuzi wa ardhi na fedha bali kuwakilisha wananchi wanaoishi naye. Wakati machifu na wakuu wa wilaya walikuwa wanaandikwa kazi katika kaunti yangu, nilimwambia gavana kwamba kila jamii inayoishi Tana River lazima iwakilishwe. Tukizungumzia kuwaachisha kazi machifu, wakuu wa taarafa au wakuu wa wilaya, haimaanishi kwamba tunataka kurekebisha au kuelekeza Wakenya kwa njia iliyo bora zaidi kuliko tulivyo sasa hivi. Tusiwe na chuki na magavana na watu wengine kwa sababu magavana ni wapita njia; leo tuna huyu na huenda kesho tukawa na mwingine. Hata wewe huenda ukawa gavana. Tunahitaji sheria dhabiti ya kuwawezesha wawahudumie Wakenya. Kwa hivyo, marekebisho yanayohitajika ni kubainisha wazi kazi ya machifu, wakuu wa taarafa na wakuu wa wilaya. Tangu waandikwe kazi, hakuna kazi muhimu ambayo wamefanya. Kazi yao ni kuwapigia debe magavana, kuenda kufanya kampeni ya magavana na kazi zingine ambazo sio zao. Huko kaunti yetu, hawa ni wale watu wakuweza kuleta amani baina ya jamii ambazo zilizozana, wale waliojisikia kwamba hawakuwakilishwa wamewakilishwa sasa hivi. Ni lazima wahakikishe kwamba watu wao wamepata maendeleo ambayo walikuwa wamekosa na walikuwa wanahitaji. Lakini haya yote yalikuwa ni kwa sababu ya wakati wa mpito. Miaka tatu iliyopita, Kenya hii tulikuwa katika mpito. Mpito ni kusema kwamba tulikuwa “ transitional period ”. Wakati huo, kila mmoja aliyeandikwa kwa kaunti au alikuwa anafanya kazi kwa kaunti, ilikuwa ni mzozano. Wawakilishi wa kaunti ambao walichaguliwa na wananchi kufanya oversight, hata hao walikuwa wakikimbia nyuma ya gavana na kufanya jambo ambalo sivyo. Lakini sasa hivi, kila mmoja ameelewa na kuwajibika ndio tunaona kila jambo la kaunti linaenda vizuri. Ndio tunaona hapa wengine wako kikaangoni. Kwa hivyo, ninaunga mkono---"
}