GET /api/v0.1/hansard/entries/674140/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 674140,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/674140/?format=api",
    "text_counter": 384,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kaunti ya Tana River na wa Mkoa wa Pwani; ninaongea lugha ya Kiswahili kwa sababu asilimia 90 ya watu wetu wanaongea Kiswahili na ninataka wanisikize na wanielewe ya kwamba leo hii, tunataka Wakenya watuelewe, yule anayefanya kazi kwa kaunti, yule anayeishi kaunti hasa ya Tana River na Pwani waelewe ya kwamba hii Seneti ni mahali pa kuhakikisha maneno ya maendeleo na ya kaunti yanaangaliwa kwa undani na hatubagui ama kuonea mtu yeyote. Kwa hivyo, kama wewe ni administrator,kama wewe ni chifu wa kata ndogo au wa kijiji, wewe sio chombo cha kukulia au “kijiko cha gavana”. Wewe ni mwakilishi wa wananchi na ni lazima uajibike. Kwa hivyo, ninaunga mkono Mswada huu kwa kupendekeza marekebisho ya kutopeleka machifu hawa nyumbani lakini tuwe na sheria kali ya kwamba wasitumike vibaya na magavana au watu wengine. Wawe mbali na siasa, ukabila, ---"
}