GET /api/v0.1/hansard/entries/674144/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 674144,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/674144/?format=api",
    "text_counter": 388,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Bule",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1029,
        "legal_name": "Ali Abdi Bule",
        "slug": "ali-abdi-bule"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, tukizungumzia administrators, tunamaanisha ya kwamba hawa tukiwa tunaita kwa lugha yoyote ile, ni watu ambao tumewaandika kutatua shida za Wakenya, wawakilishe wananchi ambao hawakuwakilishwa au walikuwa na shida tofauti hapa na pale ili tuwalete karibu na Serikali. Ugatuzi ni kuleta serikali mashinani. Kwa hivyo, walipoletewa serikali, hatutaki machifu hawa watumike vibaya na magavana. Hiyo ndiyo sababu nilisema ya kwamba wasiwe sahani au kijiko cha magavana. Wanafaa wawe watu wa kuwakilisha wananchi wanaotaka huduma kwa karibu. Bw. Spika wa Muda, tunataka marekebisho kwa machifu yawepo lakini wawekewe kwamba tukiwafuta leo, tuandike wengine. Hata mimi pengine nitakuwa gavana, na ninaweza kuwatumia vibaya. Kwa hivyo, mtu yeyote ambaye ameandikwa huko kwa kaunti kufanyia Wakenya kazi na wala sio gavana--- Kitambo Rais mstaafu, Bw. Daniel Toroitich arap Moi, alikuwa anawaambia machifu kwamba kama mambo ya usalama haitaimarika, walete sare zao za kazi. Kwa hivyo tunasema kama usalama hautaimarika na ufisadi hautatambulika, ni hao hawakuwajibika. Kwa hivyo, warudishe sare zao za kazi. Lakini tusiwafute kila baada ya uchaguzi – hawakuchaguliwa na wananchi. Wameandikwa na serikali ya wananchi. Bw. Spikawa Muda, nafikiri haya yanaeleweka kwa uwazi. Kwa hivyo, nasema kwa magavana, ole wenu. Tunasema kwamba gavana asitumie administrators kama vyombo vya kampeni. Leo hii, naona wengine wananitafuta na wengine hata sijawahi kuwaona. Wakati ambapo walikuwa wanachaguliwa, mimi nimesimama wima na kusema kila jamii lazima iwakilishwe. Mambo ya kura au kuchaguliwa si ya kuelekeza vile wananchi watachagua. Lakini haya ya kuandika, lazima tusimame imara kama viongozi kwa sababu tumeletwa hapa kwa sababu tunahitaji marekebisho na ni hili Bunge la The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}