GET /api/v0.1/hansard/entries/675013/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 675013,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675013/?format=api",
    "text_counter": 124,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Chea",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1694,
        "legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
        "slug": "mwinga-gunga-chea"
    },
    "content": "Jambo lingine ambalo ningependa kuzungumzia ni kwamba hawa wazee wetu mara nyingi huwa ndio mashahidi kule nyanjani hasa kwa kesi nyingi ambazo hutokea. Ikiwa ni kesi za watoto wetu, labda kupata mimba ama kesi za watoto kunajisiwa na masuala kama haya, wazee wetu wa vijiji ndio wako na habari hizi. Lakini ikiwa wazee hawa hawatatazamwa, ufisadi utakitili. Hakuna haja ya mzee atoke pale anaishi karibu kilomita kumi na tano kutoka mahakamani atoe ushahidi ilihali hakuna lolote atatoka nalo. Ndio maana watu watakaa chini na kuzungumza na labda mzee huyu atashikishwa kitu kidogo. Baada ya kushikishwa kitu kidogo, ushahidi hautatokea na kesi zitaanguka na hazitaenda mahali popote."
}