GET /api/v0.1/hansard/entries/675035/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 675035,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675035/?format=api",
"text_counter": 146,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwamkale",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2672,
"legal_name": "William Kamoti Mwamkale",
"slug": "william-kamoti-mwamkale"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza nampongeza Mhe. Malulu kwa kuleta Hoja hii ambayo wakati wake umefika. Hawa tunaowaita village elders sisi kule Pwani tunawaita wazee wa mtaa kwa sababu hawasimamii kijiji kama ilivyotafsiriwa; wanasimamia mtaa mzima. Ukweli wa mambo ni kwamba hawa ndio wawakilishi hasa wa Serikali kule mashinani. Hata tukitaja chief, sub-chief au Deputy County Commissioner (DCC), wote wanawategemea wazee wa mitaa kumfikia mwananchi wa mashinani ili atekeleze maagizo ya Serikali. Ukweli wa mambo ni kwamba hawa wazee wa mitaa wanafanya kazi masaa 24. Hakuna wakati ambao hawako kazini. Likitokea la mchana, lazima mzee wa mtaa atafutwe. Likitokea la usiku, lazima mzee wa mtaa atafutwe. Wakati wowote ule wanasikia amri ya chifu au DCC ili watekeleze. Hawa ni watu ambao wameacha majukumu yao. Mara nyingi mzee wa mtaa hana hata wakati wa kuenda shambani kwake, hana wakati wa kusimamia biashara yake. Amejitolea maisha yake na masaa yake yote kutumikia Serikali na wananchi. Ni jambo la kusikitisha ya kwamba mtu ataacha majukumu yake ya kibinafsi atekeleze majukumu ya umma ilhali mtu huyu hafikiriwi kupatiwa chochote. Hii ndio inachangia matatizo ya ukosefu wa usalama. Ijapokuwa tumeenda mpaka Tanzania tukaiga mambo ya wazee wa Nyumba Kumi, shida haikuwa kwamba wazee wa mitaa hawawezi kutuhakikishia usalama. Shida ni kwamba hata wanapofanya ile shughuli, wengi wanavunjika moyo ya kwamba hawapati chochote. Watoto wao wanakaa nyumbani kwa sababu hawana karo ya shule. Jamii zao zinalala njaa kwa sababu hawana chochote na wakati wao wote wanautoa kwa Serikali. Naomba hata kama tutaigiza na tuwe na wazee wa Nyumba Kumi, tusisahau kwamba kule Tanzania wazee wa Nyumba Kumi wanapatiwa kitu. Ni kwa nini tuchukue jina na tusiigize kwamba wazee hawa ni lazima waangaliwe? Nina imani ya kwamba wazee wa mitaa na wa Nyumba Kumi kama wataangaliwa na wapatiwe kitu, hii wataifanya kama kazi. Watafanya kazi hata zaidi ya wale makachero wetu na polisi wetu. Tunaposema polisi anafanya kazi masaa 24 kwa siku saba, polisi ana siku zake za kupumzika, lakini mzee wa mtaa hana siku ya kupumzika. Yeye kila wakati yuko kazini ilhali halipwi chochote. Nina imani kwamba Serikali itakapotambua na tuamue kwamba tunalipa hawa wazee wetu, shida ya ukosefu wa usalama itaisha. Mzee wa mtaa yuko pale kijijini na anaweza kukuambia ni nani mgeni aliyeingia pale hata kama ameingia usiku kwa sababu anawasiliana na wakaaji wa ule mtaa. Ni rahisi kabisa kutambua mgeni aliyeingia au mtu ambaye tabia zake si sawa. Hata hawa wezi ambao huchukua The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}