GET /api/v0.1/hansard/entries/675036/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 675036,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675036/?format=api",
    "text_counter": 147,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwamkale",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2672,
        "legal_name": "William Kamoti Mwamkale",
        "slug": "william-kamoti-mwamkale"
    },
    "content": "vitu, bila shaka wanaingiza pale katika kijiji. Usalama unatupiga chenga kwa sababu hatuwatambui, hatuwathamini wale ambao hufanya ile kazi kweli. Tunathamini wale ambao wako juu, ambao bila kuelezewa na hawa wazee wa mitaa, bila kupatiwa taarifa na hawa wazee wa Nyumba Kumi hawawezi kujua lolote. Ndio maana usalama unadorora hapa kwetu. Wakati umefika. Kama ilivyosemekana ya kwamba wazee wetu wengine wanatazama runinga saa hizi wanatusikiza tukijadili mambo yao, naomba Kamati ya Utekelezaji wachukue hili jambo kama jambo ambalo linaguza nchi nzima, linaguza wazee ambao wanasaidia kila mmoja wetu hapa. Hoja hii ya Mhe. Malulu kama itapita, basi Kamati ya Utekelezaji ichukue hili jambo na kuhakikisha ya kwamba yale tutakayopitisha hatupitishi tu kujifurahisha kama Bunge bali tunapitisha kitu ambacho kitatekelezwa. Wacha Kamati ya Utekelezaji isurutishe Serikali kutekeleza yale ambayo tutapitisha hasa haya malipo kwa wazee wetu wa mitaa, wazee wa vijiji na wazee wa Nyumba Kumi ambao tumewaleta kusaidiana na wazee wa mitaa. Naunga mkono na nina imani kwamba Wabunge wenzangu wataunga mkono wazee wetu walipwe ili watufanyie kazi hata kwa wakati huu ambao tutawahitaji zaidi. Asante, Naibu Spika wa Muda."
}