GET /api/v0.1/hansard/entries/675047/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 675047,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675047/?format=api",
"text_counter": 158,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Murungi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2802,
"legal_name": "Kathuri Murungi",
"slug": "kathuri-murungi"
},
"content": "kwa sababu tangu tulipopata Uhuru, hawajawahi kutambuliwa. Katiba asilia haikuwatambua kama viongozi. Mara nyingi, tumejadiliana nao kuhusu suala hili. Wakati Mhe. Malulu Injendi alileta Hoja hii, niliona kuwa ni busara tuichangie na kuiunga mkono ili kabla hatujavunja Bunge hili, tuwape hela ili nao wapate kiinua mgongo. Viongozi wa vijijini ndio wanachama wa mpango wa Nyumba Kumi na wametwikwa majukumu mazito sana. Hata hawapati hela zinazotoka kwa Wizara ya Ulinzi kwani zinafika tu kwa manaibu wa machifu. Labda apewe tu chai iwapo kuna kesi anashughulikia. Hawawezi kujimudu maishani na wana mahitaji mengi. Hawana nafasi ya kufanya shughuli zao kwa sababu wanatumia muda mwingi kwa kazi za wananchi. Tunafaa kupitisha haraka Hoja hii ili Kamati ya kuhakikisha kuwa sheria tunazopitisha zinatekelezwa ishughulikie Hoja hii ikiwa ya kwanza. Wana majukumu mengi sana. Wakati mwingine, mama anapotoroka mzee wake, wanaitwa kusaidia kumrudisha nyumbani. Hawalipwi mshahara. Hawana mavazi wala viatu. Wanashughulikia masuala ya nchi yetu na ni aibu kuwa tunawatumia ilhali hatuwapatii chochote. Wanafaa kulipwa mshahara mwisho wa kila mwezi. Vile vile, wanafaa kupewa sare ili unapowaona kijijini, basi utawatambua kama watu wanaotusaidia katika usalama. Wamehakikisha kuwa tuna usalama nchini. Wakati mgeni anakuja mtaani, wanafanya uchunguzi wao kirasmi na wanaweza kutueleza iwapo mgeni huyo sio mtu mzuri. Tunafaa kuwaunga mkono na kuwasaidia. Katika eneo Bunge langu la Imenti Kusini, tuna mpango wa kuhakikisha kuwa hakuna mtoto haendi shuleni. Wazee wa kijiji wametusaidia kuhakikisha kuwa wale watoto ambao wanatoroka shuleni wanajulikana na wanashika wazazi wao ili washtakiwe. Wametusaidia zaidi ya machifu na manaibu wao kumaliza pombe haramu. Vile vile, wanasaidia katika utawala wa nchi yetu. Tunafaa kupitisha Hoja hii ili tuwasaidie hao viongozi wetu."
}