GET /api/v0.1/hansard/entries/675059/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 675059,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675059/?format=api",
    "text_counter": 170,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2308,
        "legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
        "slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
    },
    "content": ", wanafanya kazi ngumu mno na wanaifanya katika umri wowote bila kupoteza hata dakika moja. Mwenyekiti wa kijiji anaanza kazi kutoka asubuhi hadi kesho asubuhi. Akiishi miaka 60, basi atakua amefanya kazi hiyo kwa takriban miaka 60, ilhali watu wengine ambao wanafanya kazi masaa manane kwa siku wanapata mishahara minono. Nataka kuwaunga mkono wale wenzangu ambao wamesema kwamba wazee wa vijiji ndio wazee ambao wanaweza kuleta shida katika usalama, na ni wao tu ndio wanaoweza kuleta nafuu kubwa katika usalama. Kila kitu kinamwangalia yeye. Ikiwa kila kitu kinamwangalia, kule kwetu wengi sana wamepigwa risasi wakionekana kwamba wanatoa siri za watu, ni watu ambao wamepata matatizo makubwa. Wanachukiana na watu kwa sababu ya kufanya kazi nzuri kwa Serikali. Lakini Serikali imewaacha nyuma. Hawajui la kufanya. Kwa hivyo, ni wajibu wetu sisi hapa tupitishe waweze kupata mshahara, na sio mambo ya kupata eti kiinua mgongo baada ya mwaka. Hapana! Tunataka wazee wa vijiji waangaliwe mapema wapate mishahara minono. Ikiwa haiwezekani basi Wabunge wajitolee kutoa mishahara ili wazee wa vijiji waweze kufaidika pia. Leo hii imekuwa vigumu wakati mwingine kwenda kukutana na wazee wa vijiji kwa sababu ukifika pale, kwa sababu ya kukosa mshahara, na unataka wafanye kazi fulani ambayo itakusaidia wewe katika kampeni zako, wanasema kwamba wao wana njaa. Sasa inatubidi sisi Wabunge tutoe pesa kutoka mifuko yetu ili tuwapatie mapeni ya kujisitiri ilhali kazi wanayoifanya ni ya Serikali. Serikali hii yetu ninajua kwamba ina uwezo wa kuwalipa wazee wote wa vijiji ndani ya taifa hili. Ikiwa wanaweza kulipa wazee kwa mwezi Kshs2,000 au kitu kama hicho, sioni sababu yoyote wasiweze kuwalipa. Wao ndio walio juu ya wale wazee ambao wamekaa majumbani na wanalipwa kila mwezi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}