GET /api/v0.1/hansard/entries/675070/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 675070,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675070/?format=api",
"text_counter": 181,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ramadhani",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2388,
"legal_name": "Suleiman Dori Ramadhani",
"slug": "suleiman-dori-ramadhani"
},
"content": "Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii nichangie Hoja hii ambayo ni muhimu sana na inahusu wazee wetu wa vijiji. Kwanza, nataka kutoa hongera kubwa zaidi kwa Mheshimiwa Malulu kwa kuokoa ndoto ambayo imesumbua sana wazee wetu wa vijiji. Kwa hakika, wazee wa vijiji ni watu muhimu sana katika taifa letu la Kenya. Kwa maoni yangu, nataka niseme ya kwamba, wazee wa vijiji ni wana muhimu zaidi ya machifu na manaibu wao, ambao wanawakilisha ofisi za utawala. Nataka niunge mkono Hoja hii moja kwa moja. Mimi ndiye muathiriwa mkubwa. Wazee wa vijiji wameathirika katika hali ya utendakazi wao wanapowakilisha mambo tafouti ambayo ni ya kiserikali. Katika Eneo Bunge la Msambweni, kuna wadi nne. Wadi moja inaitwa Gombatobongwe. Nataka kukuhakikishia kwamba wale wazee wa vijiji ambo wamepoteza maisha yao katika miaka miwili wakiwa katika taratibu za utendakazi ni zaidi ya 30. Kwa hivyo, mimi ni muathiriwa mkubwa kutokana na wazee wa kijiji waliopoteza maisha yao katika utendakazi. Kwa niaba ya watu wa Msambweni, tuko tayari kuunga mkono Hoja hii kwa kusema sio kulipwa kila mwezi peke yake, lakini ni lazima viangaliwe vipengele vingi sana ambavyo vitamwezesha yule mzee wa kijiji kwa zile huduma ambazo anapeana ziwe zinaenda sambamba na mapato yatakayotolewa. Kwa mfano, mbali na kuwa atalipwa, tumtengee mshahara mwisho wa mwezi. Vile vile, tuwe tumetenga fidia ili wakati ambapo mzee wa kijiji amepatikana na janga lolote, familia yake inaweza kupewa fidia. Pili, wale wazee wa vijiji wengi wao hawakuweza kupata masomo hapo awali. Kwa hivyo, itakuwa vyema ikiwa tukipitisha Hoja hii, wazee hao watatengewa kitengo ambacho kitawawezesha kupata masomo wakati wanatoa huduma kwa wananchi. Vile vile, naona katika ofisi ya wizara ya usalama, kumetengwa pesa za kuwanunulia machifu na manaibu wao vyombo vya usafiri. Pia itakuwa vyema wakati tunapitisha Hoja hii, wale wazee wa vijiji, tuwatambue kama viungo muhimu ili katika Bajeti yetu, wao pia wawe ni baadhi ya wale watakaonunuliwa vyombo vya usafiri. Nataka niongeze nikisema ya kwamba wazee wa vijiji ni washauri wakubwa sana katika hili taifa la Kenya kwa ajili kila jambo ambalo linafanyika katika sehemu zote za kenya linaanzia vijijini. Katika upande wa vitambulisho, upande wa mashamba na usalama, wazee wa vijiji wanafanya kazi muhimu ili kuhakikisha mambo hayo yote yamefanyika. Kwa hivyo, nawaomba viongozi wenzangu wapitishe Hoja hii. Mheshimiwa Malulu amechelewa kuuleta huu Mswada. Angekuwa ameuleta mapema, hii Bajeti ambayo imekwisha tungekuwa tayari sisi tumewajumuisha wazee wa vijiji ili waanze kupata malipo yao moja kwa moja. Kwa hivyo, nashukuru na kuunga mkono Hoja hii na vile vile, nataka nieleze ofisi ya usalama iliyo chini ya Waziri Nkaissery kwamba, kule Msambweni, katika wadi ndogo ya Gombatobongwe, wako wazee wa vijiji ambao ni zaidi ya 30 ambao wamepoteza maisha yao kwa ajili ya ukosefu wa usalama wakati walipokuwa wakifanya kazi. Lazima kuwe na taratibu ya familia za hao wazee kulipwa fidia. Isiwe watu wengine wanaofanyia Serikali kazi wanafidiwa na wazee wa vijiji hawapewi fidia yoyote, bali wanapatiwa pole na mambo yanasahaulika. Naunga mkono Hoja hii na Mungu ajalie ili ipite kwa wakati mwafaka kabla ya Bunge la Kumi na Moja halijamalizika. Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda."
}