GET /api/v0.1/hansard/entries/675216/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 675216,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675216/?format=api",
"text_counter": 117,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 128,
"legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
"slug": "richard-onyonka"
},
"content": "Asante, Dada Naibu Spika. Ukiliangalia hili jambo, wakati huu nchi ya Kenya inashtuka sana kwa sababu tuna Kamati mbili. Wakati tulipoanza kuchangia jambo hili la Tume Ya Uchaguzi na Mipaka humu nchini, vyama vya kisiasa viliketi vikakubaliana ni akina nani watakuwa wanaketi kwa kamati hiyo, Walizungumzia hili jambo ili kujaribu kutatua shida ambazo ziko katika Tume hiyo. Lakini hapo hapo, Mhe. Chepkongāa ameendelea na Kamati yake ambayo ilianza kufanya kazi hapo mbeleni. Kwa hivyo, shida iliyoko ni kuwa ingekuwa vizuri wakati utakapotoa uamuzi wako, ujaribu kuwasaidia Wakenya ili waelewa ni kwa nini tuko na kamati mbili ambazo zinazungumzia jambo ambalo kila Mkenya analiona - suala hilo moja. Nia ya kuwa na kamati mbili kujadilia hili jambo ni nini na watatatua hilo jambo namna gani?"
}