GET /api/v0.1/hansard/entries/675447/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 675447,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675447/?format=api",
"text_counter": 348,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nassir",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Ninataka nichukue mfano wangu mimi pamoja na wabunge 16 wa Seneti na Bunge la Kitaifa. Mhe. Anami alikuwa mwalimu wetu wa muziki. Leo hayuko hapa na sisi. Ninatamani, kupitia kwako Mhe. Naibu Spika wa Muda, sauti ifike kwa wakenya wengine. Tulipokuwa shuleni, wakati mmoja wafanyakazi waligoma. Wafanyakazi wote wa shule ya Lenana School ambayo ni ya kitaifa waliamua kugoma lakini kwa sababu ya ukakamavu na urafiki wa walimu, na kwamba walimu hawakuwa na ubinafsi hususan mwalimu mkuu, tulipanga kujipikia wenyewe. Chai ya asubuhi ilikuwa inapikwa na mwalimu mmoja au wawili lakini waliokuwa wanasimamia walikuwa ni wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili. Chakula cha mchana kilikuwa kinapikwa na walimu ilhali cha jioni kilipikwa na watu waliojitolea. Tuliendelea bila shida yoyote kwa muda wa takriban wiki tatu. Hakuna chochote kilichomwa wala hakuna jambo lolote lililotokea. Hii Kenya ni moja. Ninawasihi kuwa lazima turejee katika enzi zile za karne za The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}