GET /api/v0.1/hansard/entries/675618/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 675618,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675618/?format=api",
"text_counter": 141,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Mhe. Spika, ninaunga mkono Hoja hii. Tumemsikia Mhe. Gumbo vile alivyotoa maoni yake kuwa inabidi tuweke wasomi katika Kamati hizi. Mhe. Spika, nimesikia mara nyingi ukitoa mwongozo hapa Bungeni kuwa Wabunge wote wako sawa mbele ya Bunge, wawe wamesoma au bado hawajasoma, mradi tu wananchi wameona waje Bungeni. Wana haki yao ya kuwawakilisha watu wao katika sehemu wanayotoka. Ijapokuwa nimemuelewa Mhe. Gumbo yale anayoyasema kuwa angependa kuwaona wasomi peke yake, ninamuomba arudi pale tumeanzia. Kama wananchi wataona inafaa walete watu ambao kisomo chao, kulingana na Mhe. Gumbo, ni hafifu na hakilingani vile Mhe. Gumbo anavyoona, basi mimi kama mmoja wa wasomi siwezi kukaa hapa nianze kusema kuwa ninakubaliana na maoni ya Mhe. Gumbo. Tugeuze sheria iseme kuwa yeyote ambaye atakuja Bungeni lazima awe na kiwango fulani cha kisomo. Kwa sasa tunasema lazima mtu awe amefika kidato cha nne. Hicho ni kiwango ambacho tunatarajia kiwekwe ili Mbunge awe amefika kidato cha nne. Lakini ikibainika waziwazi kuwa si muhimu na wananchi wakatae waseme kuwa Mbunge yeyote mradi tu awe ni binadamu mwenye akili timamu ana haki ya kuja Bungeni, itakuwa ni uamuzi wa wananchi. Hivi sasa, tumefuata mwelekeo uliotupatia kuwa Wabunge wote wana haki sawa na ndio maana tukaleta majina haya. Ninaunga mkono Hoja hii na majina haya."
}