GET /api/v0.1/hansard/entries/675743/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 675743,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675743/?format=api",
"text_counter": 266,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shabaan",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Asante sana Mhe. Spika. Nasimama kuunga mkono Hoja hii moyo wangu ukiwa na uzito na roho yangu ikiwa na wasiwasi. Hatuwezi kufanya kazi katika Bunge hili kama wanasarakasi badala ya kama Wabunge. Sheria zetu katika Katiba zinaonyesha mujibu au kazi ya Wabunge. Tuko hapa kwa sababu Wakenya wametupatia fursa ya kuwafanyia kazi, si kwa kubahatisha. Katika hali yetu ya utendakazi, kuwa Mwanakamati ni haki ya Mbunge na ni haki ya yule anayewakilisha Wakenya ili kufanya kazi iliyopo hapa. Si sawa kuwa tunafanya kazi zetu kwa kufuatilia njia za vitendawili, sarakasi na vitimbi tukifikiria kuwa hiyo ndiyo kazi iliyotuleta hapa Bungeni. Ninastaajibika sana kuwa viongozi wa waliowachache Bungeni walitatizika sana wakiona kuwa kuna Wabunge waliochukua msimamo wa kuendelea kukaa kwenye vikao vya Kamati inayoshughulika maswala ya kisheria kwenye Bunge la Kumi na Moja na wakaanza kuwafurusha wenzao. Hivyo basi, kuna umuhimu wa viongozi wa waliowachache na waliowengi Bungeni kujua kustahamili na kujua kuwa kila mahali kuna upinzani. Hata katika jamii zetu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}