GET /api/v0.1/hansard/entries/675744/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 675744,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675744/?format=api",
"text_counter": 267,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shabaan",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "huwa kuna upinzani. Lakini bali na upinzani, ni vizuri kukaa na wenzetu na kuweza kuzungumza nao ili watu wafanye kazi pamoja na waakilishe wenzao. Nastaajibika kwamba suala la Mbunge ambaye alikuwa amekosea na kuondolewa hapa Bungeni mmelituma kwenye Kamati ya kusimamia nidhamu ya Wabunge hapa Bungeni. Hivyo basi, Wabunge wale wale ambao ni viongozi wa waliowachache, wamepiga debe na vigelegele na kuwa na furaha kwa sababu Bunge hili linalazimishwa kufanya kosa la kukubaliana na mtu ambaye alifanya makosa na katika hali ya kuadhibika, amerudishwa na korti ile. Sio kawaida kwa Wabunge wote kukimbia kortini kuwezeshwa kutekeleza kazi zao kwa niaba ya wale waliowaakilisha hapa Bungeni na kuhakikisha kuwa Wabunge watatekeleza masuala yaliyowaleta hapa kwa muhula huu, ambao ni muda wa miaka mitano. Nakubaliana kuwa si sawa kwa sisi watu wa upande wa Jubilee peke yetu kutekeleza kazi za Kamati ile kama wenzetu hawapo. Nimefurahia kuwa wanarudi kwenye kazi lakini juu ya hayo, ningeomba viongozi wa waliowachache Bungeni wajue kustahamili, uvumilivu na wajue uongozi ni kuweza kuzungumza na wenzi wao kuhakikisha kuwa Wabunge wote wanafanya kazi. Mnavyojaribu kupigia debe suala hili la yule Mbunge aliyeadhibiwa, ningependa hata nyinyi mkumbuke wale Wabunge mliowacha nje kwenye Kamati muwape nafasi wafanye kazi ili watekeleze majukumu yaliyowaleta hapa Bungeni. Naunga mkono Hoja hii."
}