GET /api/v0.1/hansard/entries/675752/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 675752,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675752/?format=api",
"text_counter": 275,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "Asante Mhe. Spika kwa kunipa nafasi kutia sauti yangu. Ijapo mengi kuhusu mawiano yamezungumzwa, pengine wenzangu hawaoni ninakoona. Wasiwasi nilio nayo ni kwamba wanaorudishwa huenda ni kwa nia ya kutumika vibaya katika Kamati hii na si kwa malengo ya kuendeleza mbele suala tulilonalo. Inawezakuwa ni kwa malengo ya kuturudisha nyuma na kutuelekeza sehemu ambayo haitatufaa kamwe. Ikiwa ni hivyo, na huyo ni pepo, ashindwe kwa jina la Yesu. Nina ombi kwa wanaorudi kwa hii Kamati. Naomba waende wakawe mabalozi wema katika Kamati na wakafanye kazi yao kwa mujibu wa sheria tupate tulichonacho mbele yetu. Suala la IEBC ni nyeti. Suala hilo linaweza kuielekeza nchi hii njia isiyofaa lisipochukuliwa kwa uzito wake. Kama wamerudishwa kwa njia njema, iwe hivyo, lakini, kama ni kwa njia isiyokuwa njema, hilo litadhihirika na tutajua ni vipi tutapambana na hali hiyo. Watu wote wakienda magharibi, mimi peke yangu nitaenda mashariki. Napinga na napinga."
}