GET /api/v0.1/hansard/entries/676251/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 676251,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/676251/?format=api",
    "text_counter": 34,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wekesa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2742,
        "legal_name": "David Wafula Wekesa",
        "slug": "david-wafula-wekesa"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nami niunge mkono Ombi hili. Najua watu wa Laikipia wameumia sana. Mzozo kati ya binadamu na wanyama pori ni jambo sugu sana hapa nchini. Naiomba Kamati ambayo inahusika na mambo ya wanyama wa porini iangalie jambo hili kwa kina sana ili binadamu aweze kukingwa kutokana na wanyama wa pori. Ninajua umuhimu wa wanyama pori hapa nchini lakini hatuwezi kulinganisha binadamu na wanyama pori. Ukitembea kote duniani utapata soko la wanyama pori lakini soko la binadamu halipatikani. Ninaunga mkono Ombi hili."
}