GET /api/v0.1/hansard/entries/676256/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 676256,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/676256/?format=api",
"text_counter": 39,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadime",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": "pori. Malalamishi ambayo yamewakilishwa na Mhe. Sara yanawaathiri watu wengi. Wale ambao mipaka yao imeshikana na mbuga za wanyamapori wanaumia, haswa, katika Eneo Bunge la Mwatate. Baada ya Standard Gauge Railway (SGR) kutengenezwa, wanyama wengi kutoka Tanzania hupitia mbuga ya Tsavo West wakitaka kwenda Tsavo East. Wanyama hawa wanazuiwa kupita Tsavo East na wote wanarejea upande wa Mwatate. Kwa sasa, jambo hili limekuwa janga kwani chakula cha wananchi kimemalizwa na wanyama hawa. Yale maji tuliyonayo kidogo yamekuwa tatizo. Juzi nimekuwa na wazo kwamba tukichimba mtaro mkubwa kabisa katika mpaka wa Tsavo, labda ndovu hawa watatumbukia humo ndani ya mtaro wakati wanajaribu kuvuka na waache kuwasumbua wananchi. Tumelia kwa muda mrefu. Waziri alikuja kule na bado hatujaona chochote ambacho kinaweza kutusaidia. Ninaomba Wizara husika iingilie kati kwani wananchi wanaumia. Ninashukuru sana kwa fursa hii mbayo umenipatia. Malalamishi ya Mhe. Sara yaangaliwe kwa undani maana ni janga la Kenya nzima."
}