GET /api/v0.1/hansard/entries/676266/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 676266,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/676266/?format=api",
"text_counter": 49,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Asante sana, Mhe Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie Ombi hili la Mhe. Sara. Tatizo la mzozo kati ya wananchi na wanyama pori limeleta shida katika Kenya yote. Kule kwetu Samburu tunaishi na wanyama. Tunachunga mifugo yetu pamoja na wanyama wa pori. Inaonekana shida iliyoko ni wananchi wanauawa na wanyama pori kama vile ndovu na mamba. Hivi majuzi, mamba alivamia watoto. Inafaa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira na Mali Asili atembee maeneo Bunge yaliyoathirika ili aelewe shida hii. Watu wanauawa na wanyama pori lakini hawalipwi fidia. Kila wakati, wanaambiwa wajaze makaratasi lakini hakuna malipo yoyote. Kuna masumbuko mengi na inafaaa Kamati itembee katika maeneo haya ili ilete ripoti Bungeni, haswa eneo la Samburu Mashariki. Tumepata habari jana kuwa kuna watoto ambao wamevamiwa na mamba. Nyoka pia wanawavamia wananchi. Masuala kuhusu mzozo kati ya wanadamu na wanyama pori yanafaa kuchunguzwa."
}