GET /api/v0.1/hansard/entries/676466/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 676466,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/676466/?format=api",
"text_counter": 249,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Injendi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2214,
"legal_name": "Moses Malulu Injendi",
"slug": "moses-malulu-injendi"
},
"content": "Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii tukijua kuwa maji ni uhai. Vile Hoja imejieleza, kiumbe binadamu lazima awe na maji. Tunaiomba Serikali kufanikisha maendeleo kama haya kwa kuwa ndiyo baba yetu. Vile mwenzangu ameeleza, hapo awali, wengi wetu tulikuwa tukichota maji mitoni. Mito mingi imechafuliwa kwa wakati huu na uchafuzi wa mazingira. Kule kwangu, mito tuliyokuwa tukitegemea sana, kama Mto Mwera na Mto Shiruma imeharibiwa. Mara nyingi, magonjwa yanakuwa mengi kwa jamii. Mito huwa mbali na jamii na tungependa maji ya mabomba ipatikane karibu na wananchi, na haswa kwa mashule. Ukienda kwa shule nyingi, baadhi ya shule ziko na maji yapatikanayo visimani. Hivyo visima vilichimbwa na kampuni ilokuwa ikiitwa Kenya-Finland Water Supply Programme (KENFICO). Kwa ajili ya idadi ya watu kuwa juu na wengine kununua mashamba, utapata jirani amechimba choo karibu na kisima. Kwa hivyo, inalazimu shule na wananchi kutoendelea kuchota maji hapo. Vile Hoja inasema, lazima tuanze kufikiria juu ya masilahi ya wanafunzi. Kwa sababu mara nyingi wanafunzi hawana maji ya mabomba. Wanafunzi hupoteza muda wao kwenda mitoni kutafuta maji. Nilivyosema, mito iko mbali. Wanapofanya hivi, wanapoteza muda wa kusoma. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}