GET /api/v0.1/hansard/entries/676467/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 676467,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/676467/?format=api",
    "text_counter": 250,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Injendi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2214,
        "legal_name": "Moses Malulu Injendi",
        "slug": "moses-malulu-injendi"
    },
    "content": "Tunaelewa wanakumbana na mambo mengi huko nje. Vijana wamekuwa chonjo na wengine wanawapachika mimba. Mzazi hufikiri mtoto yuko shuleni ilhali anapata kijana anayempa mimba wakati ameenda kuleta maji. Masomo ya msichana huwa hatarini zaidi. Hii Hoja na ile ya awali ya wazee wa mitaa zinajieleza. Ni kama tunaitisha pesa nyingi kwa Serikali. Naomba Serikali isiweke maanani mambo ya pesa bali ihudumie watu na kuhakikisha inapeana tunayouliza. Naunga mkono Hoja hii ya kuleta maji karibu na wananchi ili watoto wanaposoma, iwe ni kwa njia nzuri. Hivyo basi, watakuwa wamepata njia nzuri ya kupata kitu muhimu. Watapata chakula na maji kwa mwili. Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda."
}