GET /api/v0.1/hansard/entries/676496/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 676496,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/676496/?format=api",
"text_counter": 279,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mtengo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13164,
"legal_name": "Willy Mtengo",
"slug": "willy-mtengo"
},
"content": "Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Ningependa kuchukua fursa hii kukushukuru kwa kunipatia nafasi niweze kuichangia Hoja hii muhumi inayoshinikiza Serikali kusambaza maji kwenye taasisi za umma, zikiwemo shule za msingi. Ni dhahiri kwamba uhaba wa maji katika shule zetu ni suala nyeti linaloathiri pakubwa masomo ya watoto wetu. Nimetoka katika sehemu ambako takriban asilimia 30 ya shule hazijaunganishwa kwenye mtandao wa maji. Ni muhimu tuiunge mkono Hoja hii ili watoto wetu wapate maji masafi. Hii ni haki yao ya kimsingi ambayo inalindwa na Katiba. Ninashule ambayo watoto hutembea takriban kilomita tano baada ya kusoma, kwenda kuchota maji ndio warudi shuleni. Ni jambo la kusitikisha kwamba miaka 53 tangu Kenya ipate Uhuru bado kuna watoto ambao ni sharti watembee kilomita tano kila siku kutafuta maji. Ukosefu wa maji shuleni mwetu unaleta athari za magonjwa na hali zingine zile. Kwa hivyo, ninaunga mkono Hoja hii mia kwa mia. Ninamshukuru Mhe. Mwadime kwa kuileta Hoja hii kwa sababu itahakikisha Wakenya wengi wamepata maji masafi."
}