GET /api/v0.1/hansard/entries/676529/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 676529,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/676529/?format=api",
"text_counter": 312,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Mheshimiwa usitie wasiwasi. Utapata nafasi maana Kwale na pahali unakotoka ni tofauti. Tena wewe ni mwanaume na mimi ni mwanamke. Kwa hivyo tuko tofauti. Hoja hii imekuja wakati unaofaa lakini kwa wakati ambapo tupo katika mashaka makubwa kumaanisha ingefaa ije mapema zaidi ya hivi. Pia, ninampongeza Mhe. Mwadime kwa sababu maji ni uhai. Wakati tunazungumzia maji yaenezwe katika shule zetu, pasiwe kwamba ni shule chache. Haya maji yanahitajika sana haswa tukiangalia hali iliyo katika shule zetu na nikizungumzia sehemu za kwetu. Katika sehemu za Kinangop, Matuga na Lunga Lunga, kuna maeneo yenye ukame kwa sababu mvua haijanyesha mwaka huu. Watu wetu wako katika hali ngumu wakati huu. Watoto ndio wanaoathirika sana. Kwanza asubuhi akiamka, mzazi wake hana hata maji ya kumtengenezea kiamsha kinywa wakati anaenda shuleni ambapo anafika akiwa hana maji ya kunywa. Ukiangalia mtoto wa kike ambaye wakati wa hedhi unapofika, utakuta kwamba anahitaji maji ya kutumia kwa usafi. Kwa vile hakuna maji, yule mtoto haendi shuleni. Kusema kweli, sisi kama Bunge tunastahili kuwa na msukumo kuhakikisha maji yamepatikana bila kusema kwamba haya ni majukumu ya serikali ya kaunti. Maji ni uhai na uhai huu hauko kwa kaunti peke yake bali ni kwa nchi nzima. Ni wajibu wetu kama Bunge tuangalie katika makadirio ya ziada, tuweke pesa hapo ili wananchi waweze kupatiwa maji katika shule zetu zote. Kwa mfano, tuna huu mradi wa NYS mashinani, na nikiwa hapa ninaipongeza Serikali kwa huu mradi. Huu ni mradi ambao ungeweza kuokoa pesa kwa sababu vijana watakuwa wakisimamiwa na kufanya mambo tofauti ya ujenzi wa taifa katika maeneo tofauti. Ikiwa hizi pesa zitaekezwa katika NYS, zitatumiwa katika uchimbaji wa mabwawa, visima na mitaro ya kuweka maji karibu na shule zetu. Tukitumia vijana wa NYS, tunaweza kurekebisha paa za shule na kuweka mipangilio ambayo itaweza kukusanya maji kwa kutumia matangi. Katika maeneo yangu, shule zote hazijatenga maji ya kusaidia watoto wakati wako shuleni pamoja na walimu wao. Hii pia inachangia zaidi ukosefu wa utulivu wa watoto katika masomo."
}