GET /api/v0.1/hansard/entries/676647/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 676647,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/676647/?format=api",
"text_counter": 113,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nakara",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2926,
"legal_name": "John Lodepe Nakara",
"slug": "john-lodepe-nakara"
},
"content": "hili limekaa miaka mingi. Nawashukuru wawakilishi wa kaunti kwa bidii ambayo wamefanya ili kufikisha serikali za kaunti mahali zimefika. Jambo la kwanza ambalo ningependa kuzungumzia ni Mswada huu unatusaidia kuwapa wawakilishi wa kaunti majukumu ili wajue jinsi wanavyoweza kufanya kazi yao wakiwa na mwongozo wa kisheria na pia wakiwa na uwezo na mamlaka waliyopewa kisheria ili mtu yeyote atakayepinga uteuzi huo aweze kusimama katika sheria waliyopewa. Bunge za kaunti zinahitaji mwongozo huu ili wanapoteua watu katika nyadhifa mbalimbali wafuate mpangilio uliowekwa kisheria na mtu yeyote atakayepinga ataweza kwenda kortini na kutumia sheria hii kujipatia mamlaka. Kuna mambo ambayo ningependa kuchangia kwa ufupi. Jambo la kwanza ni kuhusu kuwajulisha wateuliwa wakati wa mchujo. Watu wengi wanaopata mwaliko kwenda mbele ya kamati za bunge la kaunti hawajui wakati wanaostahili kufika mahali pale. Lazima watu hao wajulishwe kupitia magazeti ya kitaifa ambayo yanasambazwa nchi nzima ili wajue ni lini wanatakikana kwenda mbele ya kamati za bunge la kaunti. Pia, wanapaswa kujulishwa kuhusu vitu ambavyo wanapaswa kuwa navyo wakati wa mchujo. Wakati mwingine, mteuliwa anaenda pale bila kubeba vitu vyote anavyostahili kuwa navyo kwa sababu hajajulishwa mapema kuhusu vitu anavyofaa kubeba. Ili kuwasilisha habari hizi, bunge za kaunti zinaweza kuandika barua pepe au kumpigia simu. Pia, wanaweza kumwandikia barua ili kama mtu huyo hayuko katika sehemu yenye mtandao wa rununu au redio, aweze kupata habari kupitia kwa watu wengine. Tumeona kaunti nyingi zikipoteza watu ambao wanastahili kwenda kwa mchujo kwa sababu njia za kupeana habari au za kuwafikia ni ngumu. Jambo lingine ambalo Mswada huu umetusaidia ni kuupa umma nafasi ya kuwakagua wateuliwa. Umma ndio unawajua watu kuliko maandishi. Mswada huu umeupatia umma nafasi ya kukagua watu na kupeana nafasi kwa mtu yeyote kutoa sababu za kueleza kwa nini mtu hafai kuteuliwa. Tukifanya hivi, tutapata watu ambao wanaheshimika, ambao wana sifa nzuri na ambao wanakubalika. Hata wanapopewa kazi, umma utasema ulichangia. Wakati huu ambao tuko, habari hizi lazima zifikie umma kwa njia ya magazeti ya kitaifa ili wajue wakati wanaoweza kwenda. Wakati umma unamkagua mtu, lazima pia upeane ushahidi wa ukweli kwa sababu tusipowalinda wateuliwa na kuachia umma nafasi ya kuwakagua bila ukweli au ushahidi kamili, tutapoteza watu wengi kwa njia isiyo bora. Kwa mfano, kama nilikosana na wewe au nilikushinda mahali fulani, utatumia njia hiyo ya kunipinga na kupeleka habari za uongo kwamba mimi ni mbaya. Kwa hivyo, ni lazima pia tuweke sheria kwamba shahidi yeyote ambaye anaenda kuwakilisha umma lazima awe na ushahidi wa ukweli na kama hatapeana ushahidi wa ukweli, basi sheria imchukulie hatua ili tupunguze mashahidi ambao wanatoa mambo ya uongo kuhusu mtu aliyeteuliwa. Ni vizuri tuwalinde walioteuliwa kwa sababu tukiuacha umma upeane ushahidi wa uongo, tutakuwa tunawapoteza wateuliwa wazuri."
}