GET /api/v0.1/hansard/entries/676651/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 676651,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/676651/?format=api",
"text_counter": 117,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nakara",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2926,
"legal_name": "John Lodepe Nakara",
"slug": "john-lodepe-nakara"
},
"content": "Akiambiwa sababu ya kuteuliwa kwake, mtu ataridhika. Sisi sote tunahitaji kuambiwa sababu ya kutoteuliwa kwa mtu Fulani. I lazima mtu aridhike ya kwamba hakuteuliwa kwa sababu ya jambo moja au lingine. Jambo lingine ni lile la kukataliwa kwa wateuliwa. Mswada huu unatusaidia kusema kuwa mtu yeyote ambaye anakataliwa, ni sharti apewe sababu ya kukataliwa. Nikimalizia, tunafaa kuchunga Bunge la Seneti wasichanganye wateuliwa. Kuna watu ambao wameajiriwa na lazima waendelee kufanya kazi katika kaunti. Kuna watu ambao waliajiriwa kwa muda fulani lakini kuna sheria ambayo Seneti inataka kuleta kusema kuwa baada ya miaka mitano, tunaondoa walioajiriwa na gavana fulani. Tukifanya hivyo, itakuwa siasa, tutaharibu rasilimali ya Serikali, tupoteze wakati na uwajibikaji hautapatikana. Lazima tujue kuwa magavana wamepewa mamlaka na Katiba."
}