GET /api/v0.1/hansard/entries/677025/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 677025,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/677025/?format=api",
    "text_counter": 269,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadengu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Nashukuru, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia mwelekeo. Kabla sijatoa mapendekezo yangu, wacha nifafanue kuwa niko na nia ya kugombea kiti cha ugavana katika Kaunti ya Taita Taveta 2017 lakini haimaanishi ningependa kupigania kiti cha ugavana wakati huo na sheria mbaya. Singependa niwe gavana na sheria mbaya ambayo itawafanya wafanykazi waendelee na wizi ambao ninauona. Ningependa niwe gavana ambaye atafuata sheria. Ndio maana ninapendekeza sheria hii ibadilishwe ili magavana wasiwe wanaweza kupunja na kutumia fedha za umma kiholela kama vile tunavyoona hivi sasa. Tukiangalia hali ilivyo hivi sasa, kuna mambo matatu ambayo ningependa nichangie kwa undani. Kwanza, vipengele vya 13 na 14 vinaleta vipengele vipya kabisa katika mwongozo huu wa matumizi ya fedha. Vipengele hivi vinataka Wizara ya Fedha ipewe mamlaka ya kutumia fedha za umma bila idhini ya Bunge. Naomba tukubaliane kuwa Bunge limepewa jukumu la kuidhinisha matumizi ya fedha za umma za Serikali yetu. Tukisema kuwa Wizara ya Fedha ipewe idhini ya kutumia fedha mpaka theluthi hamsini bila kupitia Bungeni, nchi hii itajikuta kwa shida. Hii ni kwa sababu italeta uzembe na maafisa wanaohitajika kuwasilisha makadirio ya pesa hawatahusika na watasema kuwa hawawezi kuwasilisha kwa muda unaofaa kwa sababu kulingana na mwongozo wa sheria za matumizi ambazo tutapitisha, zinawaruhusu kutumia fedha bila kuidhinishwa na Bunge. Napinga hicho kipengele na naomba kuleta mapendekezo yangu kuhakikisha kuwa idhini kama hiyo haitatolewa. Katika Katiba yetu, tuko na Mkaguzi wa Vitabu vya Fedha za Serikali. Ni muhimu apewe nafasi ya kukagua vitabu na kuja na sheria na miongozo ambayo itasaidia fedha za Serikali zisifujwe vile watu wanavyotaka. Tukianza kumwekea vikwazo na kumfunga kamba ya shingo ili tumwelekeze jinsi ya kukagua vitabu kwa mujibu wa sheria ambayo tunaweka, tutakua tunamnyima nafasi yake. Si ajabu kuwa hivi vitabu havitakaguliwa na vituo mwafaka ambavyo vinahitajika kuangazia vile pesa zimetumika. Si haki na sheria kumwekea Mkaguzi wa Vitabu vya Fedha za Serikali kitanzi kwani tutakuwa tunamnyima uhuru wake."
}