GET /api/v0.1/hansard/entries/677028/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 677028,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/677028/?format=api",
    "text_counter": 272,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadengu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Wenzangu wamechangia kwa undani kuhusu upotovu, kukosa nidhamu na jinsi magavana wanavyotumia pesa za umma. Ugatuzi ulikuja ili tuwe na usawa na watu wasaidike mashinani. Lakini yanayotendeka ni kuwa kandarasi zinapeanwa kiholela na hakuna makadirio ambayo yanafuatwa. Ya kusikitisha ni kuwa kuna kodi ambayo ilikuwa inachukuliwa tangu hapo awali tulipokuwa na mabaraza ya miji. Fedha hizi zilikuwa zinaonekana waziwazi. Kwa mfano, katika Kaunti ya Taita Taveta, tulikuwa tunachukua Ksh140 milioni kutoka Soko la Taveta, lakini tangu ugatuzi uingie, ada imeshuka hadi Ksh80 milioni. Shiling milioni sitini zimeenda wapi? Wanaajiri wafanyikazi na kuwalipa Kshs18,000 kwa mwezi na wanaleta kodi ya Ksh3,000. Hiyo kodi ingine haipatikani. Je, huo mshahara unaomlipa unatoka wapi? Mhe. Naibu Spika wa Muda upotovu na ukosefu wa nidhamu kama huu umeletea Kaunti ya Taita Taveta matatizo chungu nzima. Wenzangu walikuwa wanazungumza kuhusu akaunti ambazo ziko Banki Kuu ya Kenya. Unakuta kuna hundi ambazo zimetolewa za karo lakini zote zimerudi kwa sababu hakuna fedha. Ni Jambo la kusikitisha kuona kuwa kaunti inaweza kutoa fedha kupatia wanafunzi za kuwasaidia kulipa karo na hizo hundi zote zirudi kwa sababu hakuna pesa kwa akaunti. Ni jambo la kuaibisha na naomba lichukuliwe hatua ambayo inahitajika ili kuwe na nidhamu katika matumizi ya pesa za umma. Tukiwacha hawa magavana waendelee vile wanavyofanya, na nchi iendeshwe hivi, nchi hii itakwama na kusimama na hakuna lolote litaendelea kufanyika. Tutapatwa na hasara."
}