GET /api/v0.1/hansard/entries/677637/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 677637,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/677637/?format=api",
    "text_counter": 239,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi niunge mkono Hoja hii. Hoja hii ni ya muhimu sana haswa kwa sisi ambao twatoka maeneo ambayo yako na hili swala la ardhi ya jamii. Kwale inajulikana sana kuwa na matatizo ya mashamba. Tuna eneo Bunge la uwakilishi nzima; Kinango mpaka Lunga Lunga ambalo ni eneo lililotengwa kama ardhi ya jamii. Ndio maana ilipokuja Hoja ya kupitisha sheria hii, nilikuwa mmoja katika wale waliopiga kura kuiangusha maanake maslahi ya Kaunti ya Kwale hayakuwa yametiliwa maanani. Hata hivyo, baada ya kwenda katika mapatano ya Hoja hii na pia kwa sababu mimi ni mmoja kati ya wanakamati wa Kamati hiyo ya ardhi, na licha ya kuhakikisha kwamba yale mambo yanayohusu wananchi wa kawaida wa chini yametiliwa maanani, kwa hivyo, hakuna jambo la kuipinga Hoja hii tena. Kutokana na swala hilo, ndio maana ninasimama leo nikiunga mkono Hoja hii kikamilifu kusudi swala hili lihakikishe kwamba sheria hiyo ije ijadiliwe kusudi, raia ambao ni watu wa kawaida waweze kutiliwa maanani vile swala hili lilivyo. Kwa hayo machache, naunga mkono."
}