GET /api/v0.1/hansard/entries/678241/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 678241,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/678241/?format=api",
    "text_counter": 53,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Njoroge",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13158,
        "legal_name": "Ben Njoroge",
        "slug": "ben-njoroge"
    },
    "content": "Bw. Spika, naunga mkono wenzangu na hasa Seneta wa Nandi. Ninasikitika kwamba tutaenda kwenye likizo na kuacha jambo hili ambalo ni la huzuni bila kulisuluhisha. Si jambo la kuchukuliwa hivi hivi watoto wanapopotea na wengine kufariki katika Kaunti ya Nandi. Ni jambo ambalo tunatikiwa kuliangalia kwa makini. Ni jambo la kushangaza kwa sababu Wizara ya Masuala ya Nchi na Mipangilio ya Serikali inatakiwa kushughulika jambo hili na kuangazia jinsi mambo yanaendelea. Ni kinaya ikizingatiwa kwamba Waziri anayehusika na mambo ya usalama na pia Inspekta Jenerali Mkuu wako pamoja Kule Naivasha katika mafungo wakati kuna watoto ambao baadhi wamefariki na wengine kupotea. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}