GET /api/v0.1/hansard/entries/678243/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 678243,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/678243/?format=api",
    "text_counter": 55,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Nilitarajia Kamati ya Usalama wa Taifa na Uhusiano wa Kigeni kushughulikia jambo hili. Walifaa kuzuru maeneo ya kule Nandi ili kuangalia hali ilivyo kwa sababu wale in binadamu. Ni jambo la aibu sana kuona ya kwamba wale ambao wanahusika hawana lolote la kufikiria kuhusu kinachoendelea. Tunazungumza kuhusu watoto ambao waliopotea na wengine kupatikana wakiwa wamefariki. Ni vyema tupate suluhisho kabla twende kwa likizo. Ikiwa itawezekana, ni vyema tujiongezee muda hata kama ni siku mbili au tatu ili tuweze kupata suluhu kuhusu watoto ambao walipotea. Itakuwa bora kumwita Waziri anayehusika na usalama aje atueleze hapa kwa sababu hawezi kwenda kwa mafungo wakati watoto wamepotea na hakuna mtu anashughulika na jambo hilo."
}